Utangulizi
“Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, Asema BWANA”
Yeremia 30:17a.
Tukiwa sehemu ya mwili wa Kristo unaohudumia jamii kwa upendo, Idara ya Afya ya Dayosisi imejikita katika utoaji wa huduma bora za afya zenye huruma, utu na ufanisi kwa watu wote bila ubaguzi, kwa kuzingatia maadili ya Kikristo, viwango vya kitaalamu, na mahitaji ya wakati.
Majukumu ya Idara ya Afya
- Kusimamia hospitali, vituo vya afya, zahanati, na miradi ya afya chini ya Dayosisi.
- Kuratibu utekelezaji wa sera na miongozo ya afya kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali na Kanisa.
- Kuimarisha huduma rafiki kwa jamii kwa kuzingatia afya ya uzazi, watoto, vijana, wazee, na watu wenye mahitaji maalum.
- Kufuatilia ubora wa huduma za afya, matumizi ya rasilimali, na maendeleo ya watumishi wa afya.
- Kuwezesha upatikanaji wa huduma za kinga, tiba, marejeo ya rufaa, na elimu ya afya kwa jamii.
- Kushirikiana na Serikali, mashirika ya kidini, kimataifa na wadau wa afya katika miradi na program za pamoja.
Idara hii inahusisha usimamizi wa taasisi zifuatazo
Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC)
ALMC ni hospitali ya rufaa ya Kanda, inayotoa huduma za kibingwa na mafunzo kwa wataalamu wa afya. Inahudumia wagonjwa wa ndani na wa rufaa kutoka mikoa mbalimbali.
Huduma
Upasuaji wa moyo na mishipa, huduma ya dharura ya kisasa (emergency medicine), huduma ya macho, fiziotherapia, saratani, ICU, maabara ya kisasa, na huduma za kiroho.
Hospitali ya Kilutheri Selian
Selian ni hospitali yenye hadhi ya Mkoa, inayotoa huduma za kibingwa kwa jamii ya mijini na vijijini. Imejikita katika huduma rafiki kwa watu wote, hasa maskini na wasiojiweza.
Huduma
Upasuaji, huduma ya mama na mtoto, huduma za maabara, mionzi, , HIV/AIDS, kambi za upasuaji vijijini, n.k.
Vituo vya Afya na Zahanati
Dayosisi inaendesha vituo vya afya na zahanati vijijini kwa ajili ya kuhakikisha huduma zinawafikia watu wa pembezoni. Vituo hivi vinatoa huduma za msingi za afya ikiwa ni pamoja na uchunguzi, tiba, na elimu ya afya. Vituo hivyo ni; Kituo cha Afya Kirurumo, Zahanati 6 ambazo ni Arash, Piyaya, Gelai, Kitumbeine, Ilboru na Kisongo.