Idara ya Misioni na Uinjilisti

You are here:

Idara ya Misioni na Uinjilisti

Idara ya Misioni na Uinjilisti inashughulikia mambo yote ya Misioni, Uinjilisti, Uwakili na mambo yote ya Kiroho katika Dayosisi yetu. Lengo la Idara hii ni kuendeleza Agizo kuu la Utume wa Bwana wetu Yesu Kristo kama lilivyo katika Injili ya Mathayo 28:19-20.

“Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama mimi nipo pamoja nayi siku zote hata ukamilifu wa dahari“

Kazi za Idara ya Misioni na Uinjilisti

  1. Kuandaa sera ya Misioni na Uinjilisti itakayotumika katika ngazi zote za dayosisi
  2. Kuweka mikakati kati ya Wachungaji, Wainjilisti na Wakristo wote katika kutekeleza agizo la Bwana wetu Yesu Kristo
  3. Kuandaa na kuratibu mikutano mikubwa ya Kiroho ya Ki-Dayosisi, semina na warsha mbalimbali
  4. Kuhakikisha kuwa ibada, Mikutano ya Kiroho na semina zinazofanyika katika sharika za dayosisi zinafuata ta kanisa letu (KKKT)
  5. Kusimamia, kuratibu na kutoa taarifa za vitengo vyote vilivyopo chini ya idara hii na kuwasilisha taarifa hizo kwenye Halmashauri ya Misioni na Uinjilisti

Vitengo vya Idara ya Misioni na Uinjilisti

Kitengo hiki kinashughulikia mambo yote ya mafundisho ya dini katika shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Kipaimara na Ubatizo.

Kazi za Kitengo cha Elimu ya Kikristo

  1. Kusimamia na kuelekeza ufundishaji na Malezi kwa neno la Mungu katika shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Kipaimara na Ubatizo kwa kufuata utaratibu wa Kanisa letu (KKKT) na Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT).
  2. Kuhakikisha kuwepo mitaala inayotolewa na Kanisa (KKKT), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na walimu walioandaliwa vyema katika fani hiyo.
  1. Kuandaa sera ya Misioni na Uinjilisti itakayotumika katika ngazi zote za dayosisi
  2. Kuweka mikakati kati ya Wachungaji, Wainjilisti na Wakristo wote katika kutekeleza agizo la Bwana wetu Yesu Kristo
  3. Kuandaa na kuratibu mikutano mikubwa ya Kiroho ya Ki-Dayosisi, semina na warsha mbalimbali
  4. Kuhakikisha kuwa ibada, Mikutano ya Kiroho na semina zinazofanyika katika sharika za dayosisi zinafuata ta kanisa letu (KKKT)
  5. Kusimamia, kuratibu na kutoa taarifa za vitengo vyote vilivyopo chini ya idara hii na kuwasilisha taarifa hizo kwenye Halmashauri ya Misioni na Uinjilisti

Ni kitengo kinachotoa mafunzo mbalimbali ya Theologia kwa Wainjilisti na mafunzo mengine kwa wanadayosisi.

Kazi za kitengo cha Mafunzo ya Theologia kwa njia enezi

  1. Kuandaa wainjilisti kwa cheti kinachokubalika na Dayosisi na Kanisa.
  2. Kubuni na kuanzisha mafunzo ya aina mbalimbali yanayoilenga jamii kwa manufaa ya kazi ya Injili.
  3. Kuwatembelea wanafunzi katika vituo na kuwafundisha kwa utaratibu uliowekwa na bodi.

Kitengo hiki kinashughulikia mambo yote yahusuyo Kwaya, muziki, uimbaji na uenezaji wa taaluma ya muziki na uimbaji katika Dayosisi.

Kazi za Kitengo cha Uimbaji

  1. Kufundisha kwa usahihi uimbaji na muziki kwa kufuata misingi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri.
  2. Kufundisha muziki katika Majimbo na Sharika zetu zote na kuweka mkazo wa uimbaji bora wa Litrugia ya Kanisa letu.
  3. Kufuatilia, kushauri na kuratibu uimbaji katika Majimbo na Sharika.
  4. Kwaya zioneshe uchaji na nidhamu wakati wakumwimbia Mungu wawapo mahali popote, kwa maneno, matendo na mavazi yao.
  5. Kwaya zisiimbe ibadani kwa kutumia CD, VCD, DVD, VHS, Flash, memory au Audio.
  6. Kwaya zisiende popote ndani au nje ya Usharika wala kuchangisha fedha bila idhini ya Mchungaji Kiongozi.
  7. Kazi zote za sauti na video za vikundi vyote vya kwaya ndani ya Dayosisi vitasajiliwa na kulindwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni huduma katikati ya wahitaji na msingi wake ni kwenye neno la Mungu. (1Timotheo 5:1-3)

Kazi za Kitengo cha Udiakonia

  1. Kuandaa na kusimamia Sera na Miongozo ya Udiakonia kwa mujibu wa taratibu za Dayosisi yetu.
  2. Kusaidia makundi maalum kama yatima wajane na wazee
  3. Kutoa semina za kuhudumia wahitaji
  4. Kutambua wahitaji na kuwasaidia
  5. Kuwawezesha wahitaji kuweza kujitegemea wenyewe

Huduma ya Yatima na wajane Mwika (HUYAMWI).

Mtoto Yatima Maana yake nini.

Yatima ni watoto wasiokuwa aidha na mzazi moja au wazazi wote. Kuna wengine wasiokuwa hata na jamaa wa karibu. Wote hawapo.

Yatima hao walipatikana kwa sababu ya vifo vya wazazi wao vilivyotokana na ajali za kushambuliwa na wanyama wakali, vita vya wenyewe kwa wenyewe na magonjwa yaliyokosa tiba kama UKIMWI.

Huduma hii imeanza katika Dayosisi katika sharika sita za majaribio na mwaka 2017 ziliongezeka sharika zingine tano. Kwa hiyo huduma hii inaendelea vizuri. Tunapenda kutoa wito kwa sharika zote za Dayosisi kuwatambua yatima na wajane katika sharika zao, maana tukiwajua hao na kuwahudumia ndipo Mungu atakapotubariki zaidi.

Huu ni mpango wa dayosisi wa kuamsha wakristo kiroho kwa njia ya Neno la Mungu, Mikutano, Semina, Makongamano na maombi. Mkristo anapata tena nguvu na maisha mapya na kujitambua baada ya kujitathimini katika maisha na mwenendo wa kikristo.

Kazi ya Kitengo cha Uamsho

Kuamsha na kulea wakristo kiroho kwa njia ya Neno la Mungu, Mikutano, Semina, Makongamano na maombi.