Idara ya Miradi na Mali

You are here:

Utangulizi

Idara ya Miradi na Malini moja kati ya Idara tano zilizoko chini ya Halmashauri ya Mipango, Fedha na Utawala katika Dayosisi ya Kaskazini Kati. Idara hii inayohusika kuratibu, kusimamia, na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi, na Huduma.

Miradi ya Kiuchumi
  1. Hoteli
  2. Hostel
  3. Nyumba
  4. Kumbi za mikutano
Miradi ya huduma
  1. Hospitali
  2. Zahanati
  3. Vituo vya Afya
  4. Shule
Miradi ya jamii
  1. Ufugaji nyuki na Mazingira
  2. Nyumba za Mafundi na Walezi pekee/Wajane

Miradi ya Uchumi ni vitega uchumi kwa ngazi mbalimbali katka dayosisi. Lengo la miradi yote ni kutekeleza utume wa dayosisi yetu ambao ni KUMHUDUMIA MTU KIROHO, KIMWILI NA KIAKILI.

Idara hii inashughulika na masuala yafuatayo:-

  1. Kushirikiana na majimbo, sharika na Taasisi mbalimbali za Dayosisi kubuni, na kutekeleza miradi ya Uchumi na Huduma za jamii katika maeneo yao.
  2. Kusimamia na kutolea taarifa miradi ya kazi za umoja wa Kanisa zinazotekelezwa na Dayosisi.
  • Kutoa taarifa ya miradi inayofadhiliwa kutoka ndani na nje ya nchi.
  1. Kuandaa mfumo mzuri wa ushirikishwaji wa wadau katika uibuaji na uendelezaji wa miradi.
  2. Kuandaa Sera kulingana na hitaji.