Ijue Idara ya Jinsia
Idara hii inashughulikia maendeleo na mambo yote yanayohusu Wanawake na Wanaume; Kutokana na changamoto zilizopo kati ya Wanaume na Wanawake. Idara inahusisha vitengo vyote ili kuhakikisha jamii yote inaguswa na kushirikiana katika kupunguza na kuleta maendeleo Endelevu ndani na nje ya Dayosisi.
Kutokana na mgawanyiko wa majukumu ya Kijinsia Idara in vitengo viwili ndani yake ili kusaidia kufikia malengo tajwa hapo juu. Ili kufikisha huduma na kurahisisha utekelezaji wa kazi kwa kila mhitaji, Idara ina husika moja kwa moja na vitengo vyote kwa ajili ya ufanisi wa malengo tarajiwa.
Majukumu ya Idara ya Jinsia
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu wanawake na wanaume.
- Kuratibu makongamano ya maombi ya wanawake kwa majimbo.
- Kuandaa mikutano, semina, warsha na makongamano kwa wanawake na wanaume ili kupata maendeleo shirikishi na endelevu.
- Kuhakikisha haki za wanawake, wanaume, vijana na watoto hazikiukwi na uwakilishi wa jinsi zote katika vikao unazingatiwa.
- Kutoa mafundisho na elimu kwa jamii dhidi ya ndoa za utotoni, mila potofu, kazi za mikono na uwajibikaji kwenye familia unazingatiwa.
- Kuhakikisha na kuwahimiza wanaume kutimiza wajibu wao wa kufanya kazi na kutunza familia kwa kufuata maagizo ya Neno la Mungu.
- Kupokea , kuandaa na kuweka utaratibu wa maombi ya Dunia kuanzia ngazi ya Sharika.
Vitengo vya Idara ya Jinsia
Utangulizi
Kitengo cha wanawake kilianza mwaka 1973 wakati Dayosisi ya Kaskazini Kati ilipoanzishwa kutokea Dayosisi ya Kaskazini , wakati huo ikiitwa “Umoja Wa wa Wanawake Wakristo” (UWW) Sinodi Mkoani Arusha.
Wanawake ni kundi kubwa katika Kanisa kwani ni zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wote katika kanisa. Pamoja na mchango wao mkubwa katika kanisa, wanawake hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na mfumo dume uliojengeka kwenye jamii kutokana na mila potofu. Mawazo potofu ya jamii kuwa “mahali pa mwanamke ni jikoni au nyumbani” ni changamoto nyingine ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya wanawake. Kitengo cha Wanawake inaendelea na jitihada za kuwahamasisha na kuwaelimisha wanawake na jamii ili kuondokana na mawazo haya pamoja na fikra potofu ambazo zinachangia katika kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo Jamii na Kanisa kuhusu umuhimu wa wanawake katika maendeleo ya Jamii na Kanisa kwa ujumla.
Malengo makuu ya Kitengo cha Wanawake
Shughuli za Kitengo cha Wanawake zimejikita katika kuwajengea wanawake uwezo wa kiimani ambapo msingi wake ni Neno la Mungu. Wanawake pia wanajengewa uwezo wa uongozi pamoja na uwezo wa kuanzisha na kusimamia shughuli za ujasiriamali kwa lengo la kuongeza kipato na kupunguza umaskini.
Majukumu ya Kitengo cha Wanawake
Kuandaa ,kuratibu na kufundisha semina mbalimbali ili kuwajengea wanawake uwezo pamoja na kuwawezesha kupata ujuzi na maarifa katika nyanja mbalimbali.
- Kutoa elimu ya Masomo ya BIBLIA, kufanya uinjilisti pamoja na MAOMBI
- Kuhakikisha haki za wanawake hazikiukwi na uwakilishi wa wanawake katika vikao vyote unazingatiwa.
- Wanawake wa Biblia.
- Ujasiriamali; Kitengo cha wanawake kinaandaa na kufundisha ujasiriamali pamoja na kuratibu maonesho ya kazi za mikono ya wanawake.
- Kilimo cha mazao mbalimbali pamoja na bustani ya mbogamboga na miti ya matunda.
- Utunzaji wa mazingira; Wanawake wanajifunza pia juu ya utunzaji wa mazingira kwa kushirikiana na wadau wengine ili kukabiliana na wimbi la mabadiliko ya tabia ya nchi.
- Ufugaji wa kuku, mbuzi wa maziwa, na ng’ombe wa maziwa.
- Lishe bora kwa watoto, wanawake, wazee’ wagonjwa na jamii. Suala la lishe ni pamoja na kuzingatia umuhimu wa ulaji wa vyakula vya kiasili.
- Utunzaji na malezi bora ya watoto kwa kuzingatia Neno la Mungu. “Mlee mtoto katika njia ifaayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee” Mithali 22:6.
- Afya ya wanawake kuhamishi upimaji, kujitunza na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na HIV/AIDS, na Saratani ya shingo ya uzazi.
Utangulizi
Kitengo hiki kinashughulikia maendeleo na mambo yote yanayohusu wanaume katika Dayosisi
Kazi za Kitengo cha Wanaume
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu wanaume katika sharika zote ndani ya Dayosisi
- Kuomba kwa ajili ya kanisa na familia.
- Ulinzi na utunzaji wa familia
- Kuibua na kuendeleza vipawa mbalimbali walivyonavyo wanaume na kuwawezesha kuvitumia vyema katika kuendeleza Familia, Kanisa na Taifa kwa ujumla
- Kuimarisha na kuendeleza kazi za injili kuanzia ngazi ya familia
- Kupinga mila potofu zinazoathiri wanaume na wanawake kiroho, kisaikolojia, kijamii na kimwili.
Madhumuni ya Kitengo cha Vijana
- Kuwasaidia vijana wampokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
- Kuwalea vijana kimwili, kiakili na kiroho katks sharika kwa njia zifuatazo
- Ibada
- Semina za Neno la Mungu
- Makangamano na midahalo ya Neno la Mungu
- Kuwashrikisha vijana kazi za misioni ndani na nje ya kanisa
- Kuboresha maisha ya vijana kwa kuwapatia
- Semina ya ujasiriamali na kuwawezesha kuanzisha miradi midogo ya uzalishaji mali
- Kuwapa semina ya utamaduni, siasa na elimu ya afya
- Kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kanisa, maendeleo binafsi, maendeleo ya jamii na Taifa
- Kuwajengea uwezo wa kutatatu matatizo yao
Mipango ya Kitengo cha Vijana
- Kuhamasisha sharika, taasisi/idara mbalimbali, vyama vya hiari kuhusu sera ya vija KKKT/Dayosisi ya Kaskazini Kati
- Kuwainua vijana kiroho iiwawe wakristo wema wanaomkiri na kumwamini Bwana Yesu
- Kukusanya takwimu za vijana, shuhghuli zao na kuanzisha mfumo wa kubadilishana taarifa
- Kuwasaidia vijana kujiimarisha katika ajira isiyo rasmi
- Kuimarisha michezo mbalimbali (utamaduni) miongoni mwa vijana ili kukuza vipawa vya ubunifu
Utangulizi
Methali 22:6
Maono: Watu wenye furaha ,amani na Tumaini la kuurithi uzima wa milele kupitia Yesu Kristo.
Motto: Malezi na Maadili mema
Dira yetu: Kuwafikia watoto wote kwa injili , Elimu na Malezi
Dhima ya idara: Kusimamia uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya mtoto kikamilifu
MALENGO
- Kumfikia kila mtoto kwa neno la Mungu katika ukweli na usafi wote 1tim 4:12
- Kuwalea na kuwaimarisha katika maisha ya ufanisi
- Kutoa mwongozo katika maisha ya mtoto na jamii yake
- Kutoa Elimu ya kiroho za kawaida kwa watoto
- Kuwaelekeza watoto wawe wanafunzi wakati wote wa maisha yao waweze kujitegemea na kutegemewa
- Waunganishe ujuzi wa Neno la Mungu na Elimu ya kawaida Meth: 4:10
- Kuwalea katika mfumo unaojali kufikiria na kusaidia wengine
- Kuwasaidia kuboresha maisha kwa kubuni miradi midogomidogo
VITENGO
Shule ya Jumapili
Hiki ni kitengo cha msingi katika kanisa ambacho watoto wanaandaliwa ibada takatifu wakifundishwa na walimu wenye semina za walimu picha za watoto na walimu.
Shule za Awali kindagatern
Shule hizi zinafundisha kufuata muhtasari ya serikali na kanisa lengo ni kuwaimarisha watoto katika imani yao.
Compassion
Nisharika linalosaidia watoto masikini wa masikini na washirika wenza. Hivyo tuna vituo vya huduma ya mtoto 17 katika Dayosisi .
Yatima na Maskini
Sharika zetu zinatoa huduma maalum kwa watoto wahitaji na yatima huduma hizo ni Upendo Elimu na Ushauri kwa wenzio na baba na mama.